Serikali ya Japan imesema itazuia mali na kuwawekea vikwazo wanachama watatu wakuu wa Hamas.
Yoshimasa Hayashi, katibu mkuu wa baraza la mawaziri, alisema leo kwamba vikwazo vitawekwa kwenye malipo na shughuli za mtaji.
Watu hao watatu wanaaminika kuhusika katika shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na Hamas dhidi ya Israel na wanaaminika kuwa katika nafasi ya kutumia fedha kufadhili kundi hilo, msemaji mkuu wa serikali ya Japan alisema.
Japan kuweka vikwazo kwa wanachama watatu wakuu wa Hamas.
Waziri Mkuu wa Japan Kishida Fumio alilaani mashambulizi ya Oktoba 7 dhidi ya Israel na kutoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa mateka wa Hamas huku akielezea wasiwasi wake kuhusu vifo vya raia na kuzorota kwa hali ya kibinadamu huko Gaza.