Mix

Japan kwenye headlines nyingine za teknolojia, unaambiwa kwa hii miwani hakuna camera inanasa sura yako !!

on

priv2

Japan wamekuja na style mpya ya kuwasiliana kupita mitandao, ni mawasiliano bila kuonana sura…ungependa kujua inakuaje? Japan National Institute of Informatics imekuja na teknolojia mpya ya miwani inayoitwa “Privacy Glasses”.

Hii ni miwani inayoweza kuuficha uso wako mbele ya camera zozote na pia ni miwani yenye uwezo ya kuficha uso wa mtu mbele ya mashine yoyote.

priv

Ubunifu huu unaiwezesha miwani hiyo kufyonza mwanga wowote unaoipiga miwani hiyo na pia kuwezesha kuuficha uso wa mtu mbele ya camera au computer yoyote ile, kizuri zaidi ni kwamba majaribio yaliofanyika yametoa majibu chanya kwa asilimia 90% ya bidhaa hiyo.

Watengenezaji wa miwani hii wamesema bidhaa hiyo itapatikana sokoni June 2016 kwa dola 240 (Tzs. 480,000/=).

 PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments