Mix

Japan wamefungua rasmi hoteli hii mpya…huduma zake zikoje!?

on

bottom_05

Wachina na Wajapan wanajulikana kwa vitu vingi sana duniani, wakiwa miongoni mwa nchi zinazo ongoza kwa ubunifu wa Teknolojia duniani.

Nimekutana na stori kutoka Japan ambao wao wamekuja na teknolojia tofauti ya kutoa huduma za hotelini kwa kufungua rasmi hoteli ya kwanza inayoendeshwa na Marobot iitwayo Henn-na Hotel jina ambalo tafsiri yake humaanisha“Hoteli ya ajabu.”

robo

Ukifika reception utapokelewa na dada huyu, muonekano wake ni wa mwnadamu halisi, lakini huyu ni mmoja wa Robots waliopo hotelini hapo.

Hoteli ya Henn-na Hotel ipo maeneo ya Huis Ten Bosch Japan na ufikapo hotelini hapo mashine hizo za Robots zitakuwepo reception kukupokea, kukubebea mizigo au kukuhifadhia mizigo yako muhimu sehemu husika yenye ulinzi salama.

Marobot haya yana uwezo ya kuzugumza Kijapan na wageni wanaofika hotelini hapo na wana uwezo pia wa kupiga stori na mgeni bila hofu yoyote, wengine kazi yao ni kubeba mizigo ya wageni hotelini hapo, hoteli hiyo ina vyumba 72 ikiwemo chumba cha kufulia,kuhifadhia mizigo na chumba cha wafanyakazi.

Hapa chini nimekuwekea video inayo onyesha mashine hizo hapo hotelini.

 Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments