Kupitia toleo jipya la jarida la Essence, rapper P. Diddy ametokea pamoja na watoto wake wote sita kwenye ukurasa wa mbele wa jarida hilo na kuelezwa kuwa ndani yake Diddy amefunguka kuhusu maneno ya mwisho aliyoambiwa na marehemu mke wake Kim Porter.
“Siku tatu kabla ya kufariki dunia, alikuwa hajisikii vizuri, alikuwa na mafua, na aliwapeleka watoto kwenye nyumba yangu ili wasipate kuambukizwa. Usiku mmoja nilimpigia na aliniambia ‘Puffy waangalie sana watoto wangu, alisema hivyo kabla ya umauti.” >>>Diddy
Kim Porter alifariki dunia usiku wa November 15,2018 baada ya kukutwa amefariki nyumbani kwake mjini Los Angeles Marekani ambapo ilielezwa kuwa alisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya mapafu (Pneumonia) kwa zaidi ya siku saba.
Kim Porte pamoja na P Diddy walibahatika kupata watoto watatu Christian Casey Combs, Jessie James Combs na D’Lila Star Combs na kuelezwa kuwa uhusiano wao ulidumu kwa miaka 13 ambapo walianza mahusiano mwaka 1994 na kuachana rasmi mwaka 2007.
AUDIO : ULIPITWA NA HII YA FAIZA ALLY AWAKANA WATOTO WAKE KISA MPIGA PICHA “NYIE WASHAMBA HAWAKO HIVI”? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA