Habari za Mastaa

Jaji mpya kusimamia kesi ya Meek Mill ya mwaka 2008

on

Leo June 4,2019 maamuzi mapya yametolewa kuhusiana na kesi iliyokuwa ikimuandama rapper Meek Mill tangu mwaka 2008 na kuelezwa kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa upya chini ya mahakama ya Pennsylvania na Jaji mpya.

Inaelezwa kuwa mwanasheria wa Wilaya ya Philadelphia Larry Krasner aliiomba Mahakama kumpatia Meek Mill jaji mpya baada ya kuonekana maamuzi yaliyokuwa yakifanywa na Jaji Genece Brinkley yalionekana kuhusisha ubaguzi wa rangi kitu ambacho kilimuumiza Meek Mill, hata hivyo kesi hiyo itaanza kusikilizwa upya Julai 16 mwaka huu.

Inaripotiwa kuwa mwaka 2008 Rapper Meek Mill aliripotiwa kumiliki silaha kinyume na sheria ikiwemo na ishu ya matumizi ya dawa za kulevya.

VIDEO: KUMEKUCHA MISS ILALA, MASHARTI YAMETOLEWA “ATAPATA MILIONI MOJA”

Soma na hizi

Tupia Comments