Habari za Mastaa

P. Diddy kaonesha kuwa hana kinyogo na Cassie

on

Baada ya aliyekuwa mpenzi wa P.Diddy, Cassie kutangaza rasmi June 13 2019 kupitia instagram kuwa ni mjamzito na anatarajia kupata mtoto na mpenzi wake mpya Alex Fine ambaye ni mjasiriamali, Diddy hajaona tabu kuwatakia kila la kheri katika maisha yao mapya ya kuja kuwa wazazi.

Diddy ameonyesha kutokuwa na kinyongo na Cassie ingawa iliripotiwa kuwa wawili hao wamebaki kama marafiki, mkali huyo wa Hip Hop ametumia ukurasa wake wa instagram kuandikaHongera Cassie na Alex, nawatakia upendo na furaha, Mungu awabariki”. Diddy pamoja na Cassie hawakuwahi kubahatika kupata mtoto ndani ya miaka 11 ya mahusiano yao.

Inaelezwa kuwa Diddy na Cassie walikutana rasmi mwaka 2000 hii ni baada ya Cassie kujiunga na record label ya Bad Boys na ilipofika 2012 wawili hao waliamua kuweka wazi mahusiano yao lakini August 2016 inadaiwa kuwa waliachana na baadae kurudiana na October 17,2018 waliachana tena.

VIDEO: ICE BOY KAFUNGUKA ALIVYOMSAMEHE MWANAMKE WAKE ALIYEMSALITI BAADA YA KUTOKA NA RAFIKI YAKE

Soma na hizi

Tupia Comments