Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Pesa sio kitu kwa Kylie Jenner ajinunulia gari la Tsh Billioni 1

on

Baada ya Jarida la Forbes kumtaja Kylie Jenner kufikia utajiri wa dola bilioni 1 za Kimarekani miezi kadhaa iliyopita sasa ametuonyesha magari anayomiliki ikiwa pamoja na kuongeza gari lake la tano aina ya Roll Royce Phantom ambalo linatajwa kufikia thamani ya shilingi bilioni 1 za Kitanzania.

Kylie Jenner ambaye aliwahi kuzawadiwa gari aina ya Rolls Royce Classic na mpenzi wake Travis Scott kwenye siku yake ya kuzaliwa mwaka 2018 ametuonyesha kuwa gari hilo jipya analomiliki lina vitu ambavyo anavipenda ikiwemo ndani ya gari hilo kwa juu kuwa na muundo wa nyota.

Collection nzima ya magari yake kuna magari ya kifahari matano ikiwemo Mercedes Benz G Wagon, Range Rover Velar SUV, Range Rover Sports SUV, Porsche na Rolls Royce nyingine, unaambiwa kuwa thamani ya gari hizo zote inaweza kufikia kiasi cha zaidi ya Tsh. Bilioni 2 za Kitanzania.

VIDEO: MABAUNSA WAWATOA WANAFUNZI WAKIKE KWA NGUVU HOSTEL “ANA VISENTI ANAONEA WATU”

Soma na hizi

Tupia Comments