Habari za Mastaa

Baada ya miaka 27 Mary J Blige kutunukiwa tuzo ya heshima na BET

on

Inaripotiwa kuwa Mwimbaji mkongwe wa muziki wa Pop na RnB ambaye pia ni muigizaji Mary J. Blige’48 inaelezwa kuwa atatunukiwa tuzo ya heshima (Lifetime Achievement Award) kwenye tuzo za BET zitakazofanyika June 23, 2019.

Inaelezwa kuwa mwimbaji huyo ambaye aliwahi kuwa mshindi tuzo za Grammy mara tisa pamoja na kuuza album zake mara nane (multi-platinum) atatunukiwa heshima hiyo kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwenye tasnia ya muziki tangu mwaka 1992 nchini Marekani.

Mary Blige  ataungana na waimbaji kama Anita Baker wa mwaka jana, pia Charlie Wilson, Diana Ross, Whitney Houston, New Edition, James Brown na Prince wakiwa miongoni mwa mastaa waliopokea tuzo hiyo ya heshima.

VIDEO: BEN POL KAFUNGUKA SAFARI ZAKE ZA NJE, MJENGO, MAGARI YA KIFAHARI YA KWENYE VIDEO NI YA MPENZI WAKE.?

Soma na hizi

Tupia Comments