Mix

Javier Hernandez Chicharito atakiwa na vilabu sita, lakini anabaki Man United

on

chicharito_0

Wakala wa mchezaji Javier Hernandez amethibitisha kwamba mshambuliaji huyo anaendelea kubakia Old Trafford pamoja na kutakiwa vilabu sita barani ulaya.

Chacharito, 24, amekuwa akihusishwa na suala la kuondoka Manchester United ili kuweza kupata timu atakayokuwa akicheza muda mwingi.

Wakala wake Eduardo Hernandez mapema leo alikaririwa na ESPN Deported akisema: “Nilikuwa na mikutano na vilabu kadhaa, siwezi kuvitaja vyenyewe wala ofa walizotoa, wanavutiwa mno na Chicharito. Moja timu kubwa kabisa iliyopo katika Top 10 ya timu bora duniani ilikuwa moja ya vilabu sita vinavyomtaka Javier.

“Kulikuwa na klabu kutoka Germany, moja kutoka France, mbili kutoka Spain na Italy, kila timu kati ya hizo inamtaka. Lakini, mteja wangu bado yupo kwenye mkataba na Man Utd na ataendelea kuuheshimu mkataba huo.”

Tupia Comments