AyoTV

VIDEO: ‘Ningependa kushuhudia siku moja Diamond na Alikiba wakiwa pamoja’- Prof Jay

on

Ni March 17, 2017 ambapo mkongwe wa Hip Hop na mbunge wa jimbo la Mikumi Joseph Haule a.k.a Professor Jay amefunguka kuhusu maendeleo ya jimboni kwake pamoja na kutamani wakali wa Bongo Fleva Diamond Platnumz na Alikiba wafanye kazi pamoja na mashabiki zao wawe pamoja.

Akizungumza na millardayo.com & Ayo TV, Professor Jay amesema…>>>Mikumi nimefanya kazi nyingi sana moja kati ya changamoto kubwa ni maji na nimepigania Bungeni lakini pia mmeniona kwenye migogoro  mikubwa ya wafugaji kwahiyo nimekuwa nikipigana kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa lakini pia sijaacha watu wanaofanya sanaa na michezo nimewapeleka kwenye studio yangu ya Mwanalizombe’

‘Kitu kikubwa ukiongelea beef iliyopo kwenye bongo fleva ni hii ya Diamond na Alikiba nadhani mashabiki wa Diamond na Alikiba wangekuwa pamoja ili kuipigania Tanzania kwenda kwenye level nyingine nadhani muziki wetu ungeenda  mbali, kwahiyo moja kati vitu ningependa kushuhudia siku moja Diamond na Alikiba wakiwa pamoja ikifanikiwa tu hiyo naamini muziki wa Bongo unakuwa level nyingine’:-Professor Jay

VIDEO: ‘Mimi nilipataga Zero lakini sio kama sina akili’ Nuh Mziwanda, Bonyeza play hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments