Habari za Mastaa

Jay Z anafurahia mafanikio yake mtu wangu, apost ujumbe huu Twitter…

on

Rapper na Mfanyabiashara Jay Z anasababu nyingi za kusherekea matunda anayozidi kuvuna kupitia biashara zake za kimuziki… baada ya watu wengi kulalamika kuwa application ya TIDAL ya  rapper Jay Z sio biashara nzuri kwake, leo rapper huyo ana sababu kubwa ya kuamini tofauti!

TIDAL BOSS2

Jay Z amechukua time na kushare na dunia nzima kupitia page yake ya Twitter kuwa application yake ya TIDAL inayotoa huduma ya kusikiliza na download muziki imefikisha watumiaji Milion moja! Kupita page yake ya twitter rapper huyo alipost…

>>> “Kitu cha ukweli siku zote hakitishiwi, kitu ambacho hakipo hakiwezi kuwa…  watu 1,000,000 na hesabu itaongezeka. Tusherekee mafanikio haya tarehe 20/10 Brooklyn !” <<< @Mr.Carter.

JAY

Kama ulikuwa hufahamu vizuri mtu wangu iko hivi… baada ya rapper Jay Z kuinunua application ya TIDAL maneno mengi yalizuka na wengi walidai kuwa application hiyo tayari ilikuwa inaelekea kubaya na Jay Z kuwekeza hela yake kwenye hiyo huduma ni sawa na kucheza karata mbovu kwani hakuna faida atakayoivuna pale bali hasara tupu!

JAY2

Mwezi wa April Jay Z akatangaza kuwa service hiyo ina watu wasiopungua 770,000 baada ya yeye kuinunua na kuisimamia kwa mwezi mmoja tu… stori inazidi kubadilika, mwisho wa mwezi September 2015 ndio huu, kwa miezi 5 chini ya uongozi wake, application hiyo ina watumiaji  1,000,000 mpaka sasa!

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasamuziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments