Habari za Mastaa

Yule mfanyakazi aliyetoa video ya Jay Z akipigwa na Solange amefukuzwa kazi.

on

Screen-Shot-2014-05-12-at-10.22.51-PMInasemekana yule mfanyakazi ambaye aliitoa ile video inayomuonyesha rapa Jay Z akishambuliwa na shemeji yake Solange Knowles ndani ya lifti ya hotel hiyo amefukuzwa kazi.

Katika video hiyo siku hiyo Solange Knowles ameonekana kuwa na hasira mno huku akimshambulia Jay Z,ingawa mpaka sasa haijafahamika nini kilichosababisha hali hiyo kwenye lift,video ambayo ilitolewa kwa mara ya kwanza kwenye tovuti ya watu maarufu TMZ, ilimwonyesha Solange Knowles ambaye ni dadake Beyonce akimpiga Jay Z baada ya tamasha la Met lililofanyika Los Angeles Mei 5.

Baada ya ugomvi huo kwenye video mlinzi anaonekana akiingilia kati akisuluhisha ugomvi huo hata hivyo video hiyo haina sauti,Hoteli The Standard imesema kuwa ilishtushwa sana na kutolewa kwa video hiyo ambayo hukusanya matukio ya kwenye lift..

Mfanyikazi huyo amefukuzwa kazi kwa kosa la kuvunja sheria za usalama kwa kutoa video za CCTV ambazo huwa ni za siri.

Hii ndiyo hiyo video inayomuonyesha Jay Z akishambuliwa na shemeji yake.

Tupia Comments