Habari za Mastaa

Mtoto wa Jackie Chan akamatwa na gram 100 za bangi.

on

jacki

Jackie Chan ambaye aliwai kuwa balozi wa kampeni za kupinga matumizi ya dawa za kulevya amejikuta kwenye wakati mgumu na kumlazimu kuomba msamaha kwa kwa ajili yake na kwa niaba ya mwanae Jaycee Chan.

Kwenye website yake Jackie Chan ameandika, “Kutokana na swala la mwanangu Jaycee, nimekasirishwa na nimeshtushwa sana. Kama kioo cha jamii najiskia aibu sana, pia kama baba nimeumizwa sana. Mimi na Jaycee kwa pamoja tulazimika kuomba msamaha kwa jamii nzima”.

Jaycee Chan mtoto wa movie star Jackie Chan amekutwa na gram 100 za marijuana kwenye nyumba yake. Jaycee pia ni muigizaji kama baba yake.

ja

Tupia Comments