Top Stories

Ile kesi ya Bil.300, Seth wa IPTL alia na mahakama,Magereza wapewa amri (+video)

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaamuru Maofisa wa Magereza kumruhusu mfanyabiashara Harbinder Seth anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kuonana na Wakili wake kwa sababu ni haki yake.

Hatua hiyo inatokana Seth kuwasilisha madai yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kwamba ana miezi 6 hajaonana na Wakili wake kwa sababu Maofisa wa Magereza wanamkatalia kufanya hivyo.

Seth amedai anataka kuonana na Wakili wake ili waweze kuzungumzia masuala ya kesi hiyo, hivyo anaomba kibali cha Mahakama aweze kuruhusiwa kuonana na wakili wake.

Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 10, 2019 kwa ajili ya kesi kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu kesi yao haina dhamana.

Mbali na Seth mshitakiwa mwengine ni mfanyabiashara James Rugemalira ambapo wote kwa pamoja wanaokabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani Mil. 22,198,544.60 na Sh.Bil 309,461,300,158.27 kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani hapo Juni 19, 2017.

“WATOTO MILIONI 3 HAWAPO SHULENI, TUNATATUA KWA KUPAPASA” MKURUGENZI HAKI ELIMU

Soma na hizi

Tupia Comments