Habari za Mastaa

Rostam watimba na waganga redioni ‘Tumekuja na walinzi wetu’ (+ Picha )

on

Baada ya kukaa kimya kwa muda bila kuachia wimbo mpya hatimaye kundi la Rostam leo limedondosha ngoma yao mpya waliyoshirikiana na mkali Ney wa Mitego, ngoma hiyo mpya ambayo wameitambulisha kwenye kipindi cha XXL ya Clouds FM wameitambulisha kwa style ya kitofauti na vile ilivyozoeleka.

Roma na Stamina waliambata na watu ambao wamevalia mavazi ya kiganga ya kienyeji huku watu hao wakiwa wamebebelea vitendea kazi vya kiganga ambao Rostam wamewaita watu hao kuwa ni walinzi wao na kuwafananisha na kama Bodyguard wanaotumiwa na wasanii wengine wakati wakienda kutambulisha ngoma zao.

>>>“Hawa unaowaona ni walinzi wetu sio waganga na tumekuja na hawa kutokana na kile ambacho tumewaletea leo, mara nyingi wasanii wakija hapa kwenye XXL huwa wanakuja na watu waliovaa nguo nyeusi na wamenuna ila sisi tumeamua kuja na walinzi wetu wa kitofauti, kumbuka Rostam sisi tumetokea Tanga na Morogoro hivyo hawa ni mizimu yetu” Rostam

OMMY DIMPOZ KAWAJIBU WANAOMSEMA ANAPIGA PICHA NA MAGARI YA KIFAHARI

Soma na hizi

Tupia Comments