Michezo

Je Amisi Tambwe atacheza leo! Simba watoa majibu hapa

on

IMG_7718.JPG

MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Amisi
Tambwe juzi alizua hofu kwa kocha
Patrick Phiri na rais wa klabu hiyo,
Evans Aveva baada ya kuumia
mazoezi Uwanja wa Boko ,
Dar es Salaam.

Tambwe aliumia goti baada ya
kugongana na beki Abdi Banda na
kushindwa kuendelea na mazoezi hadi
akafungwa barafu baada ya kutibiwa
kwa muda na Dk Yassin Gembe.
Kocha Phiri alionekana mwenye
wasiwasi na kufuatilia kwa karibu hali
ya mchezaji huyo wakati akitoka nje. “Hakikisha anakuwa vizuri, ni
mchezaji wangu ninayemtegemea,”alisema Phiri
kumuambia Dk Gembe wakati anatoka
nje na mchezaji huyo.

Lakini sasa yakiwa yamebaki masaa kadhaa kabla ya mchezo wa Simba dhidi ya Stand United, mshambuliaji huyo aliyekuwa mfungaji bora msimu uliopita amethibitishwa kuwa fiti kuivaa timu hiyo ya Stand ambayo imepanda daraja msimu huu.

Tambwe anaweza kuanza leo kwenye safu ya ushambuliaji kwa pamoja na Emannuel Okwi.

Wakati huo huo kiungo Jonas Mkude amerejea kwenye timu baada ya kuandamwa na majeruhi kwa muda kiasi.

Tupia Comments