Tetesi za usajili wa kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Angel Di Maria kuondoka Old Trafford na kujiunga na Paris Saint Germain leo zimechukua sura mpya.
Kwa siku kadhaa baadhi ya vyombo vya habari nchini Ufaransa vimekuwa vikiripoti kwamba mchezaji huyo angeuzwa kwa ada ya zaidi ya Euro Millioni 60 na angetambulishwa rasmi na PSG Ijumaa hii, lakini kwa mujibu wa kituo cha Televisheni cha BeIN Sports kinachomilikiwa na bwana Nasser Ghanim Al-Khelaifi, ambaye mmiliki wa klabu ya PSG – ni kwamba klabu hiyo imeghairi kumsajili mchezaji huyo na mazungumzo baina ya United na PSG yameisha rasmi.
Akiwa na miaka 27, Manchester United walivunja rekodi ya usajili ya Uingereza kwa kulipa kiasi cha £59.7m kumsajili Angel Di Maria lakini muargentina huyo ameshindwa kuhimili mikikimikiki ya ligi kuu ya EPL na inaaminika anavutiwa na wazo la kwenda PSG.
Hata hivyo, inaonekana vilabu hivyo vimeshindwa kuafikiana juu, huku CEO wa United akiripotiwa kutaka kurudisha fedha zote walizotumia kumpata winga huyo.