Upepo na muamko wa kisiasa haupo nchini Tanzania tu, bali hata kwa wenzetu wa Marekani hali za kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2016 zimepamba moto huku kila mtu akizinadi ubora wa sera za Chama chake na jinsi ambavyo watatekeleza ahadi zao kwa wananchi wa Marekani.
Kama Tanzania watu wengi wa Marekani wameguswa sana na hali ya kisiasa nchini humo na miongoni wa watu walioguswa na hali hiyo ni msanii wa muziki wa Hip Hop, Young Jeezy.
Kwenye interview yake na Radio ya Hot97 iliyopo jijini New York, Young Jeezy aliulizwa kuhusu mtazamo wake juu ya hali ya kisiasa nchini humo na pia mtazamo wake kuhusu wanasiasa mbalimbali wa Marekani… Young Jeezy alikuwa na haya ya kusema…
>>> “Siku zote mimi nimekuwa msikilizaji makini kuhusu haya mambo toka nikiwa mdogo, nimekuwa na shauku ya kujua mambo yanayoendelea duniani… sasa hivi mimi ni mtu mzima, nina maisha yangu na pia ninachangia Kodi kwenye pato la Taifa, ukiachilia siasa nataka pia kujua kodi ninayolipa inatumika vipi na vitu kama hivyo, siwezi kujiita mwanasiasa ila ni muhimu kufuatilia na kuchuja sera za wanasiasa tofauti.
“Kama msanii najua jinsi gani ambavyo naweza kuwanunua watu kwa faida yangu, wanasiasa wapo hivyo pia, wengi wao wana bei ni rahisi kuwanunua kwa kutumia pesa… japo sijawahi kuwa mtu wa namna hiyo, uaminifu wangu hauwezi kununuliwa. Lakini ukifuatilia na kutazama harakati nyingi za kisiasa utagundua pesa nyingi inatumika kuwanunua wanasiasa, na vitu kama hivyo vinakufanya uitazame siasa kwa jicho la tofauti sana na pia kuwatazama wanasiasa kwa wasiwasi sana kwa sababu hujui kesho ataamkaje na atafanya nini, ni muhimu kuwa makini… “ <<< Young Jeezy.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE