Top Stories

Jeff Bezos ametangaza kuweka hili katika Utalii wa angani

on

Kampuni ya Utalii wa angani ya Blue Origin ambayo inamilikiwa na Tajiri miongoni mwa Matajiri wa dunia CEO wa Amazon Jeff Bezos, imetangaza mpango wake wa kuzindua kituo cha biashara cha angani kitwacho Orbital Reef.

.

Kukamilika kwa kituo hicho kutawapa Wateja nafasi ya kutengeneza Filamu katika eneo hilo, kufanya shughuli mbalimbali za utafiti ambapo pia kitakuwa na hoteli ya angani.

Bezos amesema wanatarajia kianze kufanya kazi kufikia mwisho wa muongo huu na watashirikiana na kituo cha angani cha Sierra na Boeing ili kujenga kituo hicho chenye ukubwa wa futi 32,000.

 

Tupia Comments