Makahama ya Misri imetoa hukumu kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi kutokana na kuuawa kwa waandamanaji wengi wakati akiwa madarakani.
Hukumu hiyo iliolewa leo kwa Rais huyo tangu aondoke madarakani mwaka 2013 kufuatia maandamano makubwa mitaani ya kupinga uongozi wake sasa amehukumiwa jela miaka 20.
Yeye pamoja na viongozi wengine wa Muslim Brotherhood walilaumiwa kwa kuwachochea wafuasi wao kumuua mwandishi wa habari na waandamanaji wa upinzani wakati wa vurugu nje ya ikulu ya nchi hiyo mwishoni mwa mwaka 2012.
Wakati umati ulipokusanyika nje ya ikulu bwana Morsi aliwaamrisha polisi kuwatawanya lakini wakakataa kufanya hivyo.
Baadaye Muslim Brotherhood waliwaleta wafuasi wao ambapo watu 11 waliuawa kwenye vurugu hizo, wengi kutoka kundi la Muslim Brotherhood.
Kabla ya kutolewa hukumu leo, Muslim Brotherhood walimlaumu rais wa sasa Abdul Fatta al-Sisi kwa kutumia mahakama kama silaha.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa>>>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.