Mchambuzi wa soka Jemedari Said Kazumari ametoa maoni yake kuhusiana na kinachoendelea baada ya Simba SC kumsajili mshambuliaji Habib Kiyombo kutokea Mbeya Kwanza, maneno yamekuwa mengi kubwa ni kauli ya Simba SC kuwa wanafanya usajili wa kutikisa Afrika, Jemedari kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika mtazamo wake kuhusiana na usajili huo.
“Habibu Kiyombo ametambulishwa Simba SC na kuzua mjadala kiasi juu ya utambulisho kamavile wa kawaida na kwamba wakati huu Fans wa Mnyama wanasubiri wachezaji wapya kingeshuka chuma kutoka nje ya Nchi halafu baadae ndo wazawa, Kyombo anaonekana wa kawaida yani, ingefaa atambulishwe maji ya jiooni sana huko.Hapa mwanzo mwanzo ni wachezaji wa Nje ndo bora”
“Lakini pia iliwahi kuandikwa kwamba huyu sio wa kustua na vitu kama hivyo almuradi Kyombo dhidi ya mchezaji yoyote wa nje ni bora huyo wa nje, ambaye pengine hata hatumjui. Nimewahi kusema tuna shida sisi kwakuwa kuanzia mashabiki, vongozi na kada nyingine wengi zao la ushabiki tu ambao kwetu cha nje ni bora kuliko cha ndani”
“Binafsi namfahamu Kyombo kitambo kabla hata hajaitwa U20 kwa mara ya kwanza na kukaa camp JKT NDEGE BEACH CLUB wakiwa na Amy Ninje. Nilijaribu kumuweka kwenye orodha ya vijana wangu lakini Kocha Amy alikuwa na mipango naye bora zaidi. Akaja kuibuka akiwa Mamelodi Sundowns ambako inaelezwa hakuwa na mkataba ule ambao ulipelekwa PSL, yes, lakini ukweli kwamba alihitajika na Sundowns na kumpa huohuo mkataba walompa, dhahiri ni kipaji kikubwa”
“Alipoamua kuja nyumbani na kujiunga na klabu za hapa kwetu kama alivyofanya LUIS MIQUSSONE, sikuona ubaya. Miquesonne nae alikuwa Mamelodi Sundowns kama Kyombo akawa anatolewa kwa mikopo hadi akarudi kwao Msumbiji. Baadae Simba wakamuona akaja kuwa Mfalme hapa Bongo”
“Ningetegemea kuona tukimsapoti kijana wetu ambaye tumeona kipaji chake tangu akiwa mdogo na kujiridhisha anaweza, kuliko mchezaji “Mzee” tusiemjua anaekuja kumalizia muda wake wa kucheza Bongo kisa tu anatoka, Rwanda, Burundi, Congo, Nigeria, Ivory Coast, Ghana, Kenya, Zambia etc etc. Huu ndo naitaga ushamba na ulimbukeni”
“SALUM ABOUBAKAR SALUM “Sureboy” amejiunga Yanga akitokea Azam FC, amekuta Aucho na Bangala pale katikati, lakini amekuja na kuweka viwango vyake pale kiasi Nabi akaamua kwenda na midundo yake na haikuwa shida Bangala kuja kucheza beki kumuachia Babu Kaju afanye mabalaa pale kati, imagine Sureboy ni Mtanzania kama Kyombo tu, ambaye hata Azam waliamini amemaliza”