Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ameagiza wahandisi mkoani humo kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kukamilisha miradi kwa ubora unaotakiwa ili waweze pia kuwavutia watu wengine hususani wanafunzi wanaopenda kuwa wahandisi.
Mtaka ametoa maagizo hayo baada ya kukagua jengo jipya la bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari Yakobi mjini Njombe ambalo limeanza kutumiwa kwa takribani miezi mitatu sasa lakini sakafu ya jengo hilo ikiwa imepasuka ndani ya muda mfupi huku Mhandisi akijitetea kuwa nyufa hizo hazina shida kwa kuwa ni za kawaida akiita Streams kwenye ujenzi.
“Kama Mhandisi anasimamia jengo linaanguka lenyewe kwa teke moja,mtoto anakaa kwenye bweni jengo limesimamiwa na “Injinia” limepasuka halafu unamwambia mtoto Engineering ni Course nzuri hawezi kukuelewa kwasababu anamuona “Injinia” ambaye anaharibu kazi,Sasa ni lazima wataalamu wetu mfanye kazi kwa weledi”amesema RC Mtaka alipofanya ziara katika Shule ya Sekondari Yakobi.