July 6 2015 ndio ilikuwa siku ya mwisho au kuvunjwa kwa baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na kuahirishwa kwa vikao mpaka baada ya uchaguzi.
Kwenye mkutano huo Jerry Silaa alitangaza kuvua madaraka ya umeya na kugombea ubunge wa jimbo la ukonga 2015 na kusema”Nimehudumu kama mstahiki meya manispaa kwa miaka mitano nafasi ya halmashauri ilikuwa ni kubwa nimemaliza salama mafanikio ni makubwa halmashauri leo hii ni kioo cha Dar es Salaam
‘kwasababu nimeongoza kwa kipindi kimoja madon wangu wananiambia ningeomba tena wangenichagua lakini nimekaa nimetafakari kwa kina nimeona budge ya halmashauri hii ni asilimia 23 ni mapato ya ndani, asilimia 77 ni luzuku ya serikali kuu kule serikali kuu inasimamiwa na bunge‘ – Jerry
‘Tunahitaji wakilishi kwenda bungeni kwenda kuiambia Serikali kuwa ilala ni zaidi ya wilaya, ilala ni zaidi ya manispaa, ilala ndio kwa hali ya kawaida inatekeleza majukumu ya makao makuu ya nchi yetu, tunahitaji fedha za kutosha, tunahitaji watendaji wa kutosha, tunahitaji mfumo wa kisasa’ – Jerry
‘Nimeamua kwa dhati kabisa kuomba Ubunge kwenye jimbo la Ukonga, naomba wananchi wenzangu wanichague moja mimi nagombea Ubunge, la pili wanichague wanaCCM wenzangu kwa kuniamini kwamba chama chetu kikinichagua mimi kwa sifa na uongozi niliyoufanya kwa zaidi ya nusu ya uhai wangu tunaweza tukashinda uchaguzi unaokuja’
‘la tatu wanichague wakiwa na nia ya kuamini kwamba mimi nikiwa mbunge wa Ukonga nitaisemea Ukonga, nitaisemea Ilala, nitaisemea Dar es Salaam na nitahakikisha Dar es Salaama inapata maendeleo endelevu’
Hii misongamano ya magari inayoonekana ni matokeo ya uwekezaji mdogo ya miundombinu Dar es Salaam, haya matokeo ya uhalifu ni matokeo usimamizi mdogo wa sheria na idadi ndogo ya Askari waliopo Dar es Salaam.Kazi hii sio ya Halmashauri, kazi hii sio ya Manispaa, kazi hii ni ya Serikali kuu kwa hiyo nadhani sasa tunahitaji watu wa kwenda kusema jinsi gani Dar es Salaam inapaswa kuendeshwa
Leo ilikuwa ni shughuli ya mwisho ya kuhitimisha baraza la madiwani lililoanza mwaka 2010 mpaka 2015 kwa kifupi tumekuja kuvunja baraza la madiwani tulikuwa na viongozi wa dini pamoja na kaimu mkuu wa mkoa kikubwa kwamba kuanzia leo mpaka mwezi wa Octoba uchaguzi utakapofanyika hakutakuwa na vikao vya baraza hakutakua na vikao vya kamati halmashauri itaendeshwa watendaji wa halmashauri na sisi tunakwenda kwenye uchaguzi.
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Jerry Slaa akizungumza kuhusu mipango mipya 2015
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie