Watu huko Gaza wananusurika kwa wastani wa mlo mmoja kwa siku huku jeshi la Israel likizuia asilimia 83 ya msaada wa chakula unaohitajika, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya mashirika 15 ya misaada.
Taarifa hiyo ilibainisha ongezeko kubwa la vikwazo vya misaada ikilinganishwa na 2023, wakati asilimia 34 ya chakula cha msaada kilizuiwa.
Amjad Al Shawa, mkurugenzi wa Mtandao wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Palestina (PNGO), aliangazia hali mbaya, akisema wakazi wote wa Gaza sasa wanategemea misaada, na uhaba huo umesababisha njaa kuenea.
“Tumezidiwa na mahitaji haya ya dharura,” Al Shawa alisema.
Mashirika yaliyohusika katika taarifa hiyo ni pamoja na Save the Children, ActionAid, Christian Aid, na Islamic Relief.