Jeshi la Israel limethibitisha vifo vya wanaume wawili ambao walichukuliwa mateka na Hamas tarehe 7 Oktoba.
“Leo, IDF ilifahamisha familia za mateka wawili Alex Dancyg na Yagev Buchshtab kwamba hawako hai tena,” Jeshi la Ulinzi la Israeli lilisema katika taarifa juu ya X.
Alex na Yagev walitekwa nyara kikatili huko Gaza na miili yao bado inashikiliwa na Hamas.
Uthibitisho wa vifo vyao umekuja baada ya ukaguzi wa kina wa kijasusi na kuidhinishwa na kamati ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya kwa ushirikiano na Wizara ya Huduma za Kidini na Polisi wa Israel.
Mazingira ya kifo chao katika utumwa wa Hamas yanachunguzwa na mamlaka zote za kitaaluma.
Tunaendelea kujitolea kukusanya taarifa kuhusu mateka huko Gaza na tutaendelea kutoa msaada kwa familia za mateka wakati huu mgumu.”