Jeshi la polisi Mkoani Geita limetoa taarifa ya kuokotwa kwa mwili wa Mtoto mdogo wa kiume anaekadiliwa kuwa na umri wa kati ya miezi nane hadi tisa ukiwa umefungwa kwenye mfuko na kutupwa jalalani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, RPC Mkoa wa Geita , Henry Mwaibambe amesema mwili wa Mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Geita kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Aidha Kamanda Mwaibambe amesema katika tukio jingine August 27,2021 katika maeneo ya Shule ya Msingi Igalula kata ya kasenga tarafa ya Kachambwa Wilaya ya Chato Mkoa wa Geita aliokotwa Mtoto mchanga wa kiume mwenye umri wa siku moja na baada ya kufanya uchunguzi imebainika Mama wa Mtoto huyo alipewa ujauzito akiwa ni Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Kachambwa.
CHANJO YALETA MADHARA KWA MIFUGO, WAMEKUFA, MIMBA ZIMETOKA, WAZIRI AWAKA “WATAFUTENI WATALAAMU”
ABIRIA WAJAWA NA TAHARUKI, WASHUKA KUPITIA MADIRISHANI KUJIOKOA NA MOTO “KAMANDA ZIMAMOTO AONGEA”