Urusi siku ya Ijumaa ilianzisha mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya Ukraine, yakihusisha makumi ya makombora na ndege zisizo na rubani, shambulio la hivi punde zaidi linalolenga kulemaza mfumo wa umeme nchini humo.
Jeshi la Urusi lililenga gridi ya nishati ya Ukraine, waziri wa nishati Herman Halushchenko aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook. “Adui anaendeleza ugaidi wake,” alisema.
Halushchenko alisema wafanyikazi wa nishati hufanya kila linalohitajika “kupunguza athari mbaya kwa mfumo wa nishati,” na kuahidi kutoa maelezo zaidi juu ya uharibifu mara tu hali ya usalama itakaporuhusu.
Jeshi la wanahewa la Ukraine liliripoti ndege nyingi zisizo na rubani zilizorushwa usiku kucha huko Ukraine zikifuatiwa na makundi ya makombora katika anga ya nchi hiyo. Ilisema Urusi pia ilitumia makombora ya balestiki ya Kinzhal yaliyorushwa kwa anga dhidi ya maeneo ya magharibi mwa Ukraine.
Shambulio la Ijumaa ni la hivi punde zaidi katika msururu wa uvamizi kama huo ambao umeongeza hofu kwamba Kremlin inalenga kuharibu uwezo wa uzalishaji wa umeme nchini wakati msimu wa baridi unaanza.
Tangu ilipoanzisha uvamizi wake mnamo Februari 2022, Urusi imeukandamiza bila kuchoka mfumo wa umeme wa Ukraine, na kusababisha kuzimwa mara kwa mara kwa vifaa muhimu vya kupokanzwa na maji ya kunywa wakati wa miezi ya baridi kali katika jaribio dhahiri la kuvunja roho ya Ukrain na kutatua