Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetoa tahadhari ya uwepo wa majanga baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kuripoti uwepo wa mvua za wastani na juu ya wastani katika baadhi ya mikoa nchini huku likiwataka wananchi kuwa makini katika kipindi hicho pamoja na kuviasa vyombo vya usafiri kutopita katika maeneo yanayopita maji kwa kasi
Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Msemaji wa Jeshi hilo,Naibu Kamishna wa Zimamoto na Uokoaji,Puyo Nzalayaimisi