Jeshi la Sudan (SAF) Jumapili lilitangaza kuwa askari 150 wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) waliuawa kwenye mapambano huko El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, magharibi mwa Sudan.
Kamanda wa askari wa miguu wa kitengo cha 6 wa SAF mjini El Fasher alitoa taarifa akisema kikosi chake kimeendelea na mapambano kwa muda wa zaidi ya saa mbili huko kusini mashariki mwa El Fasher.
Hadi sasa, baadhi ya kambi za wanamgambo ziko mikononi mwa jeshi la SAF, na idadi ya vifo vya maadui inakadiriwa kufikia 150.
Jeshi la RSF bado halijatoa taarifa yoyote kuhusu mapambano hayo