Habari za Mastaa

Picha 10 za show ya Jaguar zikiwemo za waliozimia baada ya kumuona.

on

1

6
4Kutoka 254 kwenye ardhi ya Kenyata hii story inamhusu star wa single mpya ya Kioo ambayo wiki kadhaa aliingia kwenye headlines na kuzungumziwa kuhusu video yake ambayo ameshoot na wafungwa wa ukweli  na yeye akionekana kama mmoja wa wafungwa hao.

9Hii ya leo imetokea Nakuru nchini Kenya kwenye street bash moja hivi ambayo aligusa hisia za watu wengi ambao ndio walikua wanamuona kwa mara ya kwanza.

Ni show iliyohudhuriwa na watu wengi wanaokadiriwa kuwa zaidi ya watu elfu 7 ambapo baadhi yao walizimia na kupatiwa huduma fasta kama unavyoona kwenye picha, hii ikiwa ni kutokana na mapenzi waliyonayo watu kwa Jaguar.

Miongoni mwa mashabiki hao wengi  walizimia mara baada ya kumuona tu na hiki ni kitu cha kipekee ambacho kilizoeleka kutokea kwa mastaa kama Michael Jackson.

Jaguar hupendelea kuwaita mashabiki wake wafuasi na sio mafans kama wanavyowaita wasanii wengine.

11

10

7

3

5

1Mapenzi ya mashabiki yamezidi kuongezeka sana kwake baada ya kuonekana kwamba ni mtu wa watu, tayari mpaka sasa amekua akijihusisha na ishu za kijamii kuwasaidia Wakenya mfano hivi juzi aliwalipia watu kadhaa faini iliyowawezesha kuachiwa huru kutoka gerezani, pia amekua akihudhuria misiba ya watu mbalimbali ikiwemo ya ile ishu ya nyumba kuungua na kuua watoto.

8Jaguar ambae pia anamiliki zaidi ya Tax 200 zinazobeba abiria jijini Nairobi, amekua kipenz cha wengi hasa kutokana na kuamua kushea sehemu ya kipato chake na watu wasio na uwezo na vilevile siku zote amekua mtu simple na kujichanganya na kila mtu.

Tupia Comments