Michezo

PICHA: Mashabiki wa Nantes wamejitokeza na maua kumuombea staa wao aliyepotea kwenye ndege

on

Taarifa inayoendelea kusambaa duniani kote katika upande wa soka ni taarifa kuhusiana na mchezaji wa kimataifa wa Argentina aliyekuwa anakipiga katika club ya Nantes FC Emiliano Sala kupotea kwa ndege yao binafsi aliyokuwa anasafiria yeye na rubani.

Ndege aliyokuwa ana safiri Emiliano Sala ilikuwa na watu wawili ambaye ni Sala pamoja na rubani, ndege hiyo iliyokuwa inatoka Nantes Ufaransa kuelekea katika mji wa Cardiff nchini Wales kutokana na mchezaji kutoka Nantes kuwaaga wachezaji wenzake baada ya kusaini Cardiff City, ndege yao ilipotea ikiwa katika anga la England saa chache baada ya kupaa kutokea Nantes.

Sala alisajiliwa Jumamosi iliopita na Cardiff City kwa rekodi ya usajili wa club hiyo wa pound milioni 15 lakini kufuatia taarifa za kupotea kwake na mamlaka ya anga inayofuatilia utafutaji wa ndege hiyo zinaeleza kuwa matumaini ya kuwapa Sala na rubani wakiwa hai ni mdogo sana, hivyo mashabiki wa Nantes wamejitokeza na maua kuombeleza huku wakimuombea apatikane akiwa hai.

VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”

Soma na hizi

Tupia Comments