Uongozi wa club ya Mbao FC umeripotiwa kuwa umefikia maamuzi mazito ya kumfuta kazi aliyekuwa kocha wao Ally Bushiri kutokana na kiwango kibovu alichokuwa anaendelea kukionesha akiwa anaifundisha club ya Mbao FC, uongozi umefikia maamuzi hayo baada ya Ally Bushiri kutofikia matarajio yao.
Baada ya Mbao FC kuachana na kocha wake Amri Said December 19 2018 kutokana na kutopenda kuletewa Ally Bushiri kama msaidizi wake kwa madai wana elimu sawa, walipaswa kumletea aliyejuu yake awe mkuu wake au aliyechini yake kielimu ili awe msaidizi wake, timu hiyo imeishia kushuka kwa nafasi 11 toka imeanza kuwa chini ya Ally Bushiri.
Hadi anaondoka Amri Said Mbao FC ilikuwa nafasi ya 4 katika msimamo wa TPL tofauti na sasa ipo nafasi ya 15, Mbao FC chini ya Amri Said akiwa kaifundisha Mbao FC katika game 17 za TPL, ameshinda game 6, amefungwa game 5 na ametoka sare game 6, akifunga magoli 12 na kuruhusu kufungwa magoli 16 timu ikiwa nafasi ya 4 kwa kuwa na point 24.
Amri Said alimaliza nafasi ya 6 2016/17 akiifundisha Mwadui FC na kushuka daraja na Njombe Mji akimaliza nafasi ya pili kutoka mwisho (15) 2017/18 lakini kwa sasa Mbao FC imekuwa ikiporomoka zaidi badala ya kupanda, Mbao kwa sasa ipo nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na point 36 na imecheza michezo 30 hivyo uongozi una hofu kuwa isipofanya hatua za haraka inaweza kujikuta ikiishusha timu Ligi Kuu.
Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!