Top Stories

Kesi ya Vigogo CHADEMA: Mchomelea Vyuma atoa ushahidi “Nilisikia zogo” (+video)

on

Tunayo stori kutokea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo shahidi wa pili katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa CHADEMA, Shaban Abdallah (19), amedai alimuona Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akiwahamasisha wananchi kuendelea kuandamana.

Shahidi huyo ambae ni Mchomelea Vyuma anayeishi Kinondoni Moscow ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati akitoa ushahidi wake.

Shahidi Abdallah amedai Februari 16, 2018 majira ya saa 11 jioni alikuwa dukani eneo la Kinondoni Mkwajuni alisikia zogo likisogea karibu na eneo hilo ambapo aliona waandamanaji wakiwa katika hali ya shari wakiimba ‘Hatupoi mpaka mmoja afe watatuua’ ambapo alijua ni watu wa CHADEMA kutokana na mavazi yao na bendera.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 15, 2019 ambapo washitakiwa wengine ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu,Mbunge wa Kibamba,John Mnyika,Mbunge wa Kawe,Halima Mdee,Mbunge wa Tarime Mjini,Esther Matiko,Mbunge wa Iringa Mjini,Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Vijijini,John Heche.

RIPOTI YA LHRC: “UKATILI WA KINGONO, UBAKAJI KWA WATOTO VIMEATHIRI 2018”

Soma na hizi

Tupia Comments