Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe leo September 22, 2017 amezungumza na wanahabari kwa mara ya kwanza baada ya kurudi Dar es Salaam kutoka Nairobi anakopatiwa matibabu Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi September 7, 2017 jijini Dodoma na watu wasiojulikana. Mbowe ameeleza hali ya Lissu.
"Shambulio lile halikuwa kwa Lissu peke yake, lilikuwa shambulio la Chama, kauli ya Haki, Ubinadamu na Watanzania kupitia Lisu." Mbowe.
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Lissu amebeba majeraha mengi, maumivu makali kwa kauli zake za kulitetea Taifa lake, kuwatetea Watanzania wenzake na kudai haki." Mbowe.
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Nianze na habari njema; Tundu Lissu anawasalimu sana. Nimeachana naye Nairobi jana mchana nikamwambia nitazungumza na Watanzania." Mbowe.
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Akaniomba nimpelekee salamu zake kwamba Mungu anaendelea kumpigania na In Shaa Allah baada ya muda atarejea kwa mapenzi yake." Mbowe.
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Tundu Lissu yupo chini ya ulinzi mkali sana saa 24 nje na ndani… hatuwezi kufanya uzembe tena" – FREEMAN MBOWE https://t.co/3I6O5KvNV9 pic.twitter.com/eGevH9hvL4
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Mashine yetu 'Lissu' itarudi barabarani salama kabisa ikiwa timamu, nataka niwaeleze ufahamu wake uko vizuri 100%" https://t.co/3I6O5KvNV9 pic.twitter.com/n5Yd16xRXp
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Lissu hakukata kauli mpaka anaingia theatre, pamoja na majeraha yote hajawahi kukata kauli" – MBOWE LIVE >>> https://t.co/6SREALIZDv pic.twitter.com/qYyoh7zBAH
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Hali ya mgonjwa, Lissu alifikishwa Nairobi usiku saa sana, hali yake ilikuwa ngumu sana. Madaktari walitupokea na kuanza kumhudumia." Mbowe
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Madaktari wanasema ni miujiza kutoka salama bila kukatwakatwa kwa risasi ktk shambulio kama la Lissu"-MBOWE LIVE >> https://t.co/6SREAM0B25 pic.twitter.com/19X8a73p6E
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Lissu anatibiwa na kundi kubwa la madaktari na ningependa niwatambue waingie kwenye rekodi kwa kazi ya ziada kuokoa maisha ya Lissu." Mbowe
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Kabla ya madaktari wa Nairobi, niwashukuru madaktari wa Hospitali ya Dodoma. Kama wasingefanya wajibu wao wa msingi tusingesafiri na Lissu"
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Kazi kubwa iliyofanywa na madaktari wa dodoma tusiipuuze, ilituwezesha kufika Nairobi akiwa hai. Ilikuwa ni miujiza kila mmoja alishangaa."
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Ikasemwa Ndege ya Lissu imelipiwa na wanaCCM, hata ingelipiwa na CCM bado si shida ila ukweli imelipiwa na CHADEMA" https://t.co/6SREAM0B25 pic.twitter.com/WRtsAaPH6X
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Kuna presha ya kumpeleka nchi tofauti sita; wapo waliotaka apelekwe A. Kusini, wengine India, Ubelgiji, Ujerumani, UK na USA" Mbowe
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Kama kiongozi wa Chama nadiriki kusema kwamba mshukiwa namba moja wa shambulio la Lissu ni vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi hii" Mbowe.
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Hilo nalisema bila kumung'unya maneno, viashiria vyote vya tukio lile tangu linatokea kauli na kusita kwa viongozi na kauli za kujiosha."
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Ni nani katika vyombo vya ulinzi na usalama, simjui lakini ni vigumu sana kusema tukio la ujambazi, hakuna ujambazi pale." Mbowe.
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Watu wetu wamepotea, watu wetu wameuawa, wanapigwa risasi mchana kweupe na hakuna hatua ya maana inayofanyika." Mbowe.
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Michango ya TZ ni mil.52, mil.43 zilizochangwa Bungeni bado hatujapewa, wa Marekani wamemchangia Lissu USD 20000" https://t.co/6SREAM0B25 pic.twitter.com/w6w3iyUV7T
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Nimalizie kwa gharama za matibabu. Hakuna kificho kila kitu kimewekwa humu. Mpaka juzi gharama zilifikia Ksh Milioni 6.7." Mbowe.
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
"Ksh Milioni 7.4 ni sawa na Tsh Milioni 162.8 kwa wiki mbili za matibabu lakini tunasema hata zingekuwa Bilioni, zimemuokoa Lissu." Mbowe.
— AyoTV (@ayotv_) September 22, 2017
Ulipitwa na hii? BREAKING: CHADEMA baada ya Serikali kukubali kumgharamia Lissu
Hii je? Mipango ya kumpeleka TUNDU LISSU Marekani imesimamishwa