Ijumaa ya January 12 2018 katika mitandao ya kijamii zimeenea taarifa za kusikitisha kuhusu staa wa zamani wa soka wa kimataifa wa Nigeria aliyewahi kuvichezea vilabu mbalimbali Ulaya Wilson Oruma kuripotiwa kuwa amepata ukichaa.
Oruma ameripotiwa kupata ukichaa baada ya kutapeliwa na mchungaji (Pastor) wake Naira bilioni 1.2 ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 75 za kitanzania, ambapo mchungaji huyo alimshauri Oruma ampatie pesa hizo ili wafanye uwekezaji katika biashara ya mafuta.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Wilson Oruma licha ya kuiongoza Nigeria U-17 kama nahodha na kutwaa Ubingwa wa dunia 1993, amewahi kuvichezea vilabu mbalimbali Ulaya kama Olympique Marseille, Sochaux, Servette na Lens.
Alichokifanya Simon Msuva kwa Wakati Ujao Youth Academy