Michezo

Neymar hajaridhishwa na penati waliopewa Man United

on

Usiku wa March 6 2019 jijni Paris Ufaransa ulichezwa mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League kati ya Man United dhidi ya Paris Saint Germain ambao ndio wenyeji wa mgame hiyo, PSG waliingia kucheza game hiyo wakiwa mbele kwa magoli 2-0 waliyoyapata katika mchezo wa kwanza.

Game ya marudiano mchezo ulibadilika na kujikuta PSG wakipoteza mchezo huo nyumbani kwa kufungwa kwa magoli 3-1, (agg 3-3) ila wamejikutaka wakiaga michuano hiyo kutokana na wao wameruhusu kufungwa kwa magoli mengi nyumbani kwao.

Goli la mwisho lililowapeleka hatua ya robo fainali Man United ndio lilizua gumzo lililopatikana kwam penati iliyopigwa na Marcus Rashford sekunde chache kabla ya game kuisha kwa madai ya Kimpembe wa PSG alishika mpira katika eneo la 18, baada ya kutolewa Neymar ambaye anakosekana kwa kuwa nje ya uwanja kwa majeruhi, amelaumu na kueleza kuwa ile haikuwa penati.

“Hata kama wakichukua watu wanne ambao hawajui mpira na wafutilie kwa picha za marudio za video taratibu, sio kweli (penati) ni namna gani (Kimpembe) alitumia mkono wake kwa nyuma kwa kuufuata mpira”>>>>Neymar Via Instagram

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

Soma na hizi

Tupia Comments