Top Stories

VIDEO: Kinachomfanya Bongo Zozo asite kuomba uraia wa TZ, Maisha yake?

on

Moja kati ya watu waliojizolea umaarufu mkubwa wakati wa fainali za mataifa ya Afrika 2019 nchini Misri kwa upande wa Tanzania ni pamoja na Nick Reynolds maarufu kwa jina la Bongo Zozo kuamua kujitolewa kuishabikia timu ya taifa ya Tanzania kwa moyo wote kama vile anashabikiwa taifa lake la asili la England.

Bongo Zozo ambaye ni raia wa England baada ya kuenea mitandaoni na lugha yake ya Kiswahili cha mtaani kama mtanzania wa kawaida, alifanya mahojiano na AyoTV na kueleza kuwa anakwama kufikiria kuchukua uraia wa Tanzania kwa sababu anahofia kuwa akichukua ataukosa uraia wa England ambao yeye anatumia passport ya UK kama chombo cha kusafiria.

Nick ameweka wazi kuwa ikitokea siku Tanzania itaruhusu uraia wa nchi mbili basi atakuwa katika mstari wa kwanza kuomba uraia wa Tanzania kwa sababu ni nchi anayoipenda, kwani akibadili na kuwa na uraia wa Tanzania na kupoteza wa UK itamuwia vigumu kusafiri kwa urahisi tofauti na alivyokuwa na passport ya Uingereza.

VIDEO: Tanzania yatolewa kinyonge AFCON, Hii ndio kauli ya Samatta

Soma na hizi

Tupia Comments