Kabla ya kufunga mwaka wa 2015, staa wa muziki kutoka Wondaland Records, Jidenna alizisogeza kwetu ngoma tatu mpya; Extraordinaire, Chief na Knickers. Time hii staa huyo wa ‘Classic Man‘ anaileta rasmi official music video ya ‘Knickers’.
Wimbo wa Classic Man umefanikiwa kuchaguliwa kwenye kipengele cha Best Rap/Sung Collaboration kwenye Tuzo za Grammy’s… lakini kwa sasa Jidenna bado yupo studio akikamilisha album yake ya kwanza inayotarajia kuwa sokoni very soon.
>>> “Mtegemee vitu vizuri. Mtegemee album yenye miondoko kama ya Classic Man. Mtapata fursa ya kusikia na kujua ni vitu gani anavyofanya mtu yoyote ambaye ni Classic Man…. mtegemee moja ya album kali kwa mwaka wa 2016…” <<< Jidenna aliuambia mtandao wa Rap-Up Tv.
Itazame official music video ya Knickers kwenye hizi dakika 5 hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.