Habari za Mastaa

Ugeni mpya kwenye familia ya mwigizaji Jim Iyke…

on

Mwigizaji wa Nollywood Nigeria Jim Iyke ana sababu kubwa sana ya kutabasamu na kufurahi siku ya leo. Baada ya kumpoteza mama yake mzazi kipindi kama hiki mwaka jana staa huyo wa movie anafungua ukurasa mpya wa furaha maishani mwake.

jim-iyke2

Jim Iyke na mpenzi wake.

Jim Iyke na mpenzi wake wa mwaka mmoja wamemkaribisha duniani mtoto wao wa kwanza wa kiume kwenye hospitali ya Grady Hospital iliyopo jijini Atlanta Marekani.

Jim-Iyke

Jim Iyke alikuwa na haya ya kusema kuhusu baraka za kupata zawadi ya mtoto mwaka huu..

>>>“Ni mwaka jana tu nilikuwa na huzuni mkubwa baada ya kumpoteza mama yangu mzazi lakini leo, mwaka mmoja badaae nina machozi ya furaha”. <<< Jim Iyke.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments