Timu ya Taifa la Tanzania Taifa Stars asubuhi ya leo July 18, 2017 imefanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Taifa Stars itaondoka Mwanza July 19 kuelekea Kigali, Rwanda kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Taifa la Rwanda na wachezaji wote wamefanya mazoezi ya pamoja kasoro beki Shomary Kapombe ambaye alikuwa akifanya mazoezi maalum na jopo la madaktari wa timu.
Kama utakumbuka Shomary Kapombe alipata majeraha yaliyomlazimu kutolewa uwanjani mapema katika mchezo wa kwanza dhidi ya Rwanda uliomalizika kwa sare ya 1-1.
Ayo TV na millardayo.com zimempa daktari wa Taifa Stars, Richard Yomba na kutaka kufahamu hali ya Shomary Kapombe.
“Kimsingi Kapombe kabla alikuwa na tatizo la nyonga kwa hiyo akawa amepata matibabu akawa yupo vizuri bahati mbaya ile mechi iliyopita kama tulivyoona kama tulivyoona watanzania akatonesha majeraha yake hatuna namna tutamuacha katika safari.” – DR Yomba.