Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Jibu la Amunike kuhusu ishu za kumpa kazi Okocha ndani ya Taifa Stars

on

Baada ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kuifunga Uganda 3-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi L wa AFCON 2019 na kufuzu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39, zilizuka tetesi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Emmanuel Amunike atamteua mnigeria mwenzake Jay Jay Okocha kuwa msaidizi wake katika fainali hizo za AFCON 2019 nchini Misri.

Amunike amekanusha taarifa hizo kupitia TBC 1 na kusema ni uzushi tu “Okocha sio kocha wala simtafuti kocha mpya na hata kama nina mpango wa kuongeza watu watakuwa wanaongeza kitu timu ya taifa, sasa Okocha sio kocha unawezaje kumleta sio kweli watu wanapenda kuongea na kila mtu yupo huru kuongea anachopenda na kutoa maoni yake”

Okocha

Taifa Stars mwezi June 2019 itakuwa Misri katika fainali za AFCON 2019 ambazo droo yake inapangwa April 12 2019, kama utakuwa unakumbuka vizuri Okocha na Amunike walicheza pamoja timu ya taifa ya Nigeria kwa miaka 8 (1993-2001)

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments