Mix

Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete imeokoa hizi milioni za matibabu nje ya nchi

on

Leo January 17 2017 Mkurugenzi wa upasuaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ‘JKCI’ ambaye pia ni Daktari Bingwa Upasuaji wa Moyo  Dkt. Bashir Nyangasa amezungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyotokana na upasuaji wa moyo wagonjwa 6 katika taasisi hiyo.

Dkt. Nyangassa amesema Taasisi hiyo  imeokoa kiasi cha shilingi Milioni 174 kwa kuwafanyia  upasuaji wa moyo wagonjwa 6 katika taasisi hiyo

>>>’Kwa mwaka 2017 tumeanza kwa kufanya kambi ya kwanza ya upasuaji kwa kushirikiana na timu ya wataalamu kutoka hospitali ya Apollo, Bangalore ya nchini India na kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa sita (6) kati ya hao wanaume ni wanne na wanawake wawili’-Dkt. Nyangassa

Dkt.Nyangasa alifafanua kuwa kama Serikali ingewasafirisha wagonjwa hao 6 kwenda kupata matibabu nje ya nchi gharama ya shilingi milioni 174 ingetumika ambapo kwa kuwafanyia wagonjwa hao hapa nchini gharama ambayo imetumika haizidi shilingi milioni 60.

Mkurugenzi wa Tiba ya Moyo JKCI Peter Kisenge alisema kuwa Taasisi hiyo  inategemea kupokea madaktari kutoka  Afrika na Saudi Arabia kwa  ajili ya upasuaji wa kutanua mishipa ya moyo iliyoziba, kutanua milango ya moyo iliyoziba na kuziba matundu ya moyo. 

Kambi ya madaktari wa Afrika  itakuwepo katika Taasisi hiyo kuanzia tarehe tarehe 23  mpaka 29 mwezi huu, ambapo wagonjwa 15 watafanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua(Catheterization Procedure).

VIDEO: Kwa mara ya kwanza hospitali ya Muhimbili ilivyoweza kuweka betri kwenye moyo wa mtoto, Bonyeza play hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments