Michezo

Kwa walipofikia Man United wanamuhitaji Zlatan Ibrahimovic

on

Pamoja na kuwa Zlatan Ibrahimovic ametangaza kuwa yuko mbioni kurudi LaLiga kwa maana ya Hispania kupitia ukurasa wake wa instagram, staa wa zamani wa Man United Paul Ince ameweka wazi kuwa kwa sasa Man United wanamuhitaji Zlatan Ibrahimovic.

Zlatan amedaiwa na Ince kuwa kwa namna Man United ilivyo sasa inamuhitaji mchezaji huyo kurudi Man United na kwenda kuwa kiongozi, Zlatan anakaribia kumaliza mkataba wake na LA Galaxy ya Marekani na sasa Ince anaona staa huyo licha ya kuwa na umri wa miaka 38 ila anahitajika Old Trafford.

“Zlatan ameonekana kutoa taarifa kama anarudi Hispania na kwingine kuwa anaendelea kucheza MLS, nafikiri kwamba kama atapenda kurudi Man United itakuwa ni njia nzuri kwake pia, atakuwa ni mzuri na muhimu kwa kuelimisha wachezaji wote vijana na ushawishi”>>>Paul Ince

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Zlatan Ibrahimovic amewahi kuvichezea vilabu mbalimbali barani Ulaya kama Inter Milan, AC Milan, FC Barcelona na hata Man United aliyowahi kuichezea kwa miaka miwili (2016-2018).

AUDIO: Edo Kumwembe aeleza kocha anaestahili kuwa Yanga sio Zahera

Soma na hizi

Tupia Comments