Michezo

Bodi ya Man United imemkubali Ole Gunnar Solskjaer

on

Baada ya kuwa na mwanzo mzuri akiwa kama kocha wa muda Man United Ole Gunnar Solskjaer sasa uongozi wa club ya Man United licha ya kupoteza game ya Ligi Kuu weekend iliyomalizika dhidi ya Arsenal kwa kupoteza kwa goli 2-0, wamepanga kumpa rasmi mkataba wa kudumu ndani ya Man United.

Taarifa hizo zimetolewa na mitandao mbalimbali leo kuwa Man United imepanga kumtangaza Ole Gunnar Solskjaer kama kocha wa mpya mkuu, wakati wa mapumziko ya michezo ya vilabu weekend hii na kucheza michezo ya timu zao za taifa iliyopo katika kalenda ya FIFA.

Ole Gunnar Solskjaer toka amejiunga na Man United December 2018 kama kocha wa muda wa timu hiyo akimrithi Jose Mourinho, amepoteza michezo miwili tu ya mashindano yote ambazo ni game dhidi ya Arsenal ya Ligi Kuu na Champions League dhidi ya PSG, akiwa kaiongoza kwa zaidi ya game 15.

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

Soma na hizi

Tupia Comments