Michezo

Ujumbe wa kwanza wa Ronaldo kwa wareno baada ya kutolewa World Cup

on

Jumamosi ya June 30 2018 ilikuwa ni siku ya kihistoria kwa mashabiki wa soka wa Ureno na mashabiki wa Cristiano Ronaldo kwani ni siku ambayo safari ya Ureno kwenda kutwaa Kombe la Dunia ilihitimishwa rasmi na timu ya taifa ya Uruguay.

Ureno alicheza mchezo wake wa hatua ya 16 bora ya World Cup 2018 dhidi ya timu ya taifa ya Uruguay katika uwanja wa na kujikuta akikubali kipigo cha magoli 2-1, magoli ya Uruguay yote mawili yakifungwa na Edinson Cavani dakika ya 7 na 62 wakati goli la Ureno lilifungwa na Pepe dakika ya 55.

Baada ya kipigo hicho Cristiano Ronaldo alitumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe huu kwa wareno ambao ndio walikuwa wanaisapoti timu yao “Sapoti yenu imekuwa na itakuwa msingi wa sisi kufanya vizuri siku zote asanteni Ureno”

Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake

Soma na hizi

Tupia Comments