Mix

Taarifa nyingine kuhusiana na hali ya kiafya ya Rais Kikwete.

on

Miraj IITaarifa kuhusiana na hali ya kiafya ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete ambaye yupo Maryland Marekani kwa ajili ya matibabu, imesema hali yake kiafya inaimarika na ameanza mazoezi ya kutembea ikiwa ni siku ya pili tangu afanyiwe upasuaji wa tezi dume.

Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imetoa taarifa hiyo na kuongeza kuwa itaendelea kutoa taarifa kadri hali yake itakavyokuwa inaendelea.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mtoto wa Rais Kikwete, Miraj Kikwete (@kikwete) ameweka picha muda mfupi uliopita inayomwonyesha Rais pamoja na maneno haya;- “… #26464 #we #good TABASAMU TU LEO . thank you everyone for your endless support, love and prayers. It means so much to Dad, myself and our family. You are a strength to us. TUNAWASHUKURU KWA KUJALI ….

Miraj

Miraj AA

 

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments