Habari za Mastaa

Umekisikia walichokizungumza Jokate na Wema baada ya tukio la Arusha kipo hapa.

By

on

wemaKama ni mfatiliaji mzuri wa maisha ya mastar hawa wa Tanzania bila shaka utakuwa umekiona au kukisikia kilichotokea Arusha kwenye tamasha la Divaz Night with Mirror ambalo wawili hawa waliwashangaza watu waliokuwepo kwenye ukumbi huo wakifatilia burudani hizo.

Jokate na Wema ilitoka taarifa kuwa hawapatani kutokana na kile kilichoonekana kuingia kwenye mahusiano nacDiamond Platnumz ambaye amewahi kuripotiwa kutoka na Jokate kipindi cha nyuma.

wema2Wema amezungumzia jinsi alivyopokea kwa namna Jokate kum’sapraiz’ jukwaani ambapo amesema>>’Mimi mwenyewe nilishangaa kwa sababu nilikuwa sijui lakini nilishamwambia Jokate kuna kitu Dar na Arusha,kwa sababu mi na yeye hatuna bifu na sasa ni marafiki wa karibu’

‘Kwa hiyo tulivyokuwa tunachat kabla hata ya show nilimwambia J’mosi ya kuamkia February 01 kwaArusha kutakuwa na kitu cha furaha akanambia basi sawa,nikamuuliza nikuweke kwenye matangazo akasema no nikufahamisha kwa hiyo mpaka mwisho wa siku nikajua labda siku hiyo hatokuja’

‘Lakini bila kutegemea maskini alikuja akaja kuni’Sapraiz’  tukashow love,nikiwa jukwaani nikaambiwa Jokate yuko ndani ya ukumbi nikaona nimtangaze angalau aje kutoa salaam kwa mashabiki,alivyokuja maskini kumbe alikuja kunitunza akawaambia watu nimekuja kumtunza mke mkubwa’.

Kipaza sauti kilienda kwa Jokate nae alizungumza haya>>’Aliniomba kama wiki 3 zilizopita niende nae kwenye Arusha alikua na Anti Ezekiel na kina Jaq wolper lakini nilikua sina hakika na ratiba yangu baadae ilivyokaribia nikaona ni kitu kizuri kum’sapraiz’ kwa sababu kuna watu wanafikiri tuna bifu kwa hiyo nikim’sapraizi’ kitu kinakuwa na mvuto zaidi nilisema kama shamrashamra kuchangamsha shughuli yake’.

wema3Bonyeza play kumsikiliza Wema sepetu akielezea jinsi alivyoipokea hali hiyo na kuhusu bifu yao.

Hapa Wema akielezea bifu yao.

Malizia story kwa kumsikiliza Jokate aka Kidoti.

Tupia Comments