Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameendelea na ziara ya Dar Mpya ambayo lengo ni kutafuta majibu ya kero mbalimbali zinazo0wakabili wananchi.
Leo November 27 2016 ikiwa ni siku ya tisa ameanza ziara yake katika wilaya ya Kindondoni kabla hajakutana na wananchi amezungumza na watendaji mbalimbali wa Manispaa ya Kinondoni na haya ni baadhi ya mambo ambayo ameyazungumza.
'Moja ya changamoto tuliyonayo ni matumizi mabaya ya ofisi kwa wenyeviti wa mtaa'-RC Makonda #DarMPYA #KINONDONI
— millardayo (@millardayo) November 27, 2016
'Ni marufuku mwenyekiti wa mtaa kutembea na mhuri, mhuri unakaa ofisini na unakuwa chini ya mtendaji'-RC Makonda #DarMPYA #KINONDONI
— millardayo (@millardayo) November 27, 2016
'Nitapeleka maombi kwa Rais kwa ajili ya kuwapunguza watumishi, hatuwezi kuwa na watu ambao kazi yao ni kula tu'-RC Makonda #DarMPYA
— millardayo (@millardayo) November 27, 2016
'Kuna watendaji hawawezi kufanya kazi mpaka wasikie DC anapita au ugeni unakuja, wengine wanacopy na kupaste ripoti'-RC Makonda #DarMPYA
— millardayo (@millardayo) November 27, 2016
'Hata uwe unafahamiana na kigogo yeyote kama hufanyi kazi tutakung'oa, serikali hii siyo ya kujipendekeza'-RC Makonda #DarMPYA #KINONDONI
— millardayo (@millardayo) November 27, 2016
'Kila mtendaji akitimiza majukumu yake kazi ni rahisi sana'-RC Makonda #DarMPYA #KINONDONI
— millardayo (@millardayo) November 27, 2016
'Utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji Kinondoni umesababisha kuwa na barabara nyingi za lami ambazo ni feki'-RC Makonda #DarMPYA #KINONDONI
— millardayo (@millardayo) November 27, 2016
'Moja ya maeneo yaliyooza kinondoni ni upande wa ujenzi, mmetujengea mtaro mbovu'-RC Makonda #DarMPYA #KINONDONI pic.twitter.com/e6VK7oCV9T
— millardayo (@millardayo) November 27, 2016
'Nataka kujua wale wakandarasi waliojenga barabara chini ya viwango, hatua gani mmechukua'-RC Makonda #DarMPYA #KINONDONI pic.twitter.com/bsxSlkKBRh
— millardayo (@millardayo) November 27, 2016
'Maafisa elimu mnajisikiaje mpaka DC atoke aende akabaini madudu mashuleni wakati nyie mpo'-RC Makonda #DarMPYA #KINONDONI pic.twitter.com/iZpyVxWkLZ
— millardayo (@millardayo) November 27, 2016
'Kiongozi wa juu akibaini madudu kwenye idara yako wakati wewe upo, tunakung'oa'-RC Makonda #DarMPYA #KINONDONI pic.twitter.com/7ZdtAczeVH
— millardayo (@millardayo) November 27, 2016
ULIKOSA? Wakazi wa Mloganzila walivyosimama barabarani kuzuia msafara wa RC Makonda, UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI