Michezo

Pep Guardiola ameomba radhi leo na kutaja timu anayoishabikia UEFA

on

Baada ya ushindi wa kishindo wa Man City dhidi ya Schalke 04 na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya UEFA Champions League msimu wa 208/2019, kocha mkuu wa Man City Pep Guardiola kuelekea michezo ya mwisho ya FC Bayern na Liverpool ameweka wazi atashangilia timu ipi.

Leo kwenye Champions League utachezwa mchezo wa FC Bayern dhidi ya Liverpool mchezo ambao utachezwa nchini Ujerumani baada ya game ya kwanza Liverpool wakiwa nyumbani kutoka sare ya 0-0, hivyo kila timu itahitaji ushindi walau wa goli moja ili kusonga mbele.

Hivyo kocha wa Man City Pep Guardiola amekuwa tofauti na wengi kwa kusema ataishangilia Bayern licha ya kuwa kwa sasa anafanya kazi na kuishi England, hivyo waliamini kuwa atatangaza kuwa ataishangilia Liverpool ifuzu na sio FC Bayern ambayo amewahi kuifundisha kwa miaka mitatu (2013-2016).

“Samahani kwa watu wa England ningependa kuona Bayern Munich ikisonga mbele, mimi ni shabiki wao na sehemu ya hii club ambayo walinipa fursa ya miaka mitatu kuishi nchini Ujerumani, naipenda Munich, naipenda Bayern na watu wake wote kwa sababu nina marafiki wengi pale, napenda Bayern wafuzu lakini sio rahisi maana hii ni game yenye uhitaji wa matokeo kwa wote”>>>Guardiola

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke 

Soma na hizi

Tupia Comments