Habari za Mastaa

Vazi la JLO wakati akifanya tamasha lafika kwa Waziri mkuu wa Morocco..

on

mp

Miongoni mwa mastaa ambao mara nyingi wamekuwa gumzo kwa mashabiki wao kutokana na uvaaji wa nguo zao za nusu utupu wakati wakiwa jukwaani ni majina ya Jennifer Lopez, Nick Minaj na Beyonce huwezi kuyakosa.

Kuna nchi ambazo hawaangalii sana suala la uvaaji wa mastaa wakiwa stejini lakini hii imemkuta Jennifer Lopez wakati akifanya tamasha lake katika mji wa Rabat, Morocco ambapo unaambiwa Serikali ya nchi hiyo imeingilia kati baada ya kuonekana ni sawa na kuwadhalilisha wanawake.

Waziri mkuu wa Morocco  Abdelilah Benkirane ametaka kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu matangazo yaliyokuwa yakirushwa live na Tv ya Taifa wakati wa tamasha la mwanamuziki huyo.

lop3

Tamasha hilo ambalo lilifanyika Mei 29 la miaka 10 ya Mawazine lilifanyika huko Rabat na kurushwa live na kituo cha televisheni cha 2M, Waziri huyo amesema watafanya uchunguzi kutokana na picha zilizoonyeshwa kukiuka sheria za nchi kutokana na kutokuwa na maadili.

lop2

Waziri wa mawasiliano wa nchi hiyo alilaumiwa kwa kuruhusu tamasha hilo kurushwa kupitia televisheni ya Taifa na kulikuwepo na tetesi za kutakiwa kujiuzulu kutokana na kitendo hicho.

Waziri mkuu ametaka waliohusika kwa kushindwa kuingilia kati na kuzuia kuonyeshwa kwa picha hizo wachukuliwe hatua.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

 

Tupia Comments